Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kulinda mazingira ya bahari ikiwemo kupiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki inayotumika, kudhibiti kwa asilimia 99 uvuvi haramu pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za uvuvi wa bahari kuu.
Wachimbaji wadogo Wisolele kupata umeme ifikapo Oktoba
Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini, usimamizi na utunzaji wa mazingira ya Bahari inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanzia Julai 19 hadi 27 mwaka huu, amesisitiza kwamba ni lazima kuzuia na kupunguza uchafuzi wa bahari kwa kila namna kuanzia vyanzo vya ardhini hadi baharini.
Aidha, amesema kwa sasa katika kulinda bahari vinahitajika vitendo zaidi vitakavyokwenda sambamba na sayansi, uvumbuzi na teknolojia pamoja na ushirikishwaji wa wadau wote unaojumuisha vijana na wanawake katika mijadala ambao ni sehemu ya suluhu.