Serikali yaeleza chanzo cha kifo cha mwandishi wa TBC aliyefia Ml. Kilimanjaro

0
59

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Joachim Kapembe amefariki kwa ajali ya baiskeli wakati akitoka katika kituo cha Kibo kuelekea kituo cha Horombo baada ya kupanda kufika kileleni mwa Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza na TBC, Msigwa amemuelezea mwandishi huo kuwa ni mmoja wa watu ambao hawakupatwa na athari za kupanda mlima (mountain sickness) na alifanya kazi yake vizuri ikiwemo kurekodi na kuhoji watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Nape Nnauye.

“Baada ya kufanikiwa kufika kileleni Kilimanjaro na kushuka watu wote tulifika kambi ya Kibo ambako tulipaswa kuendelea kwenda kambi Horombo, wachache waliamua kutumia baiskeli badala ya kutembea kwa miguu akiwemo Joachim Kapembe. Bahati mbaya akiwa anateremka, mteremko wa kutoka Kibo ndipo akapata ajali iliyosababisha apoteze maisha,” ameeleza.

Waziri Mkenda: GPA isiwe kigezo pekee cha ajira vyuo vikuu

Msigwa ametoa pole kwa familia, wafanyakazi wa TBC, waandishi wa habari, ndugu jamaa na marafiki na kueleza kuwa “Joachim Kapembe alikuwa mwandishi wa habari mahiri, aliyekuwa anajiamini, mchapakazi, mzalendo, mwenye nidhamu, muadilifu na aliyependa kufanya kazi kwa ushirikiano.

Send this to a friend