Serikali yaeleza chanzo cha mafuriko Hanang

0
51

Serikali imesema chanzo cha mmomonyoko wa ardhi wilayani Hanang mkoani Manyara ni kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ulikuwa na miamba dhoofu iliyonyonya maji na kusababisha maporomoko, hivyo kutengeneza tope.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema Serikali ilifuatilia taarifa za matetemeko kuanzia Septemba mwaka huu hadi siku ya tukio na kubaini kuwa hakukuwa na tetemeko lolote wala mlipuko wa volcano.

“Uchunguzi huu umefanywa na wataalam wetu na bado wanaendelea kufanya uchunguzi zaidi ili kuendelea iwapo eneo hili linakabiliwa na tukio hili zaidi,” amesema Matinyi.

Rais Samia akatisha safari ya Dubai kushughulikia maafa Hanang

Amesema kati ya watu 65 waliopoteza maisha, miili 60 tayari imechukuliwa na wapendwa wao kwa ajili ya taratibu za maziko huku miili mitano ikiwa bado haijatambuliwa ambapo Serikali inafanya taratibu za kufanya vipimo vya DNA ili iweze kutambuliwa.

Aidha, Serikali imewaasa wananchi, taasisi na wadau mbalimbali kujitoa kwa hali na mali ili kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo ikiwemo vyakula, mafuta, madawa ma kadhalika kupitia akaunti ya maafa ya taifa, namba 9921151001 ‘Maafa Hanang’

Send this to a friend