Serikali yaendelea kukarabati shule kongwe nchini

0
49

 

Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara ni miongoni mwa shule kongwe nchini Tanzania, shule inayosifika kwa kufundisha wanafunzi kwa vitendo lakini pia ufaulu mzuri katika matokeo yake.

Katika kuhakikisha shule hizi kongwe zinabaki kuwa bora serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imewezesha shule hii kuongezewa madarasa mawili kupitia mpango wa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Madarasa hayo yaliyojengwa shuleni hapo yamekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wenye ulemavu, kwani darasa moja wanalitumia kwa ajili ya kujifunzia muda wa ziada lakini pia darasa jingine linasaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Wanafunzi wa shule hiyo wamemshukuru Rais Samia kutokana na ujenzi huo kwani umetoa ahueni ya kujifunza kwa uhuru zaidi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Riyadh Kadhi pia ametoa shukrani zake kwani wanafunzi wake ambao wana mahitaji maalum wanaweza kupata muda
mzuri na nafasi ya kukaa na walimu wakasoma muda wa ziada.

Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara ni miongoni mwa shule nyingi amabazo zimenufaika na ujenzi wa madarasa nchi nzima, Serikali ilito apesa na kuhakikisha madarasa 15,000 yamejengwa nchi nzima ili kupunguza tatizo la upungufu wa madarasa lililopelekea wanafunzi
kubanana pamoja ujenzi wa shule mpya katika baadhi ya kata.

Send this to a friend