Serikali yafungulia magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa

0
50

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametoa leseni kwa magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa, ambayo ni Mwanahalisi, Mseto, Tanzania Daima na Mawio.

Ameyasema hayo katika semina na Wahariri wa vyombo vya habari leo mkoani Dar es Salaam katika mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuendesha na kusimamia vyombo vya habari katika maadili na taaluma ya uandishi wa habari.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake, Mkurugenzi wa Gazeti la Mwanahalisi na Mseto,  Saed Kubenea ameanza kwa kumshukuru Rais na waziri kwa kuanza ukurasa mpya na vyombo vya habari.

Licha ya neema hiyo kuna uwezekano wa magazeti yasiwepo mtaani kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyopo.

“Kuna magazeti ambayo hayakufungiwa lakini yamejifungia yenyewe kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyopo. Serikali iangalie namna ambavyo itaweza kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari binafsi,” amehimiza Kubenea.

Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa tayari wameanza kutekeleza kuwepo kwa ratiba za uwezeshaji wa mafunzo kwa waandishi wa habari..