Serikali yafuta baadhi ya tozo za miamala kwa maelekezo ya CCM

0
56

Serikali imesema kuwa haina malengo ya kuwatoza wananchi wake kodi au tozo kwa ajili ya kuwapa mzigo, bali inalenga kuwahusisha Watanzania wote kwa umoja wetu katika juhudi za kujiletea maendeleo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo bungeni jijini Dodoma ambapo ameeleza kuwa Serikali imefuta na kupunguza baadhi ya tozo baada ya kufanyika mapitio.

Ametaja tozo zilizofutwa kuwa ni tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote), tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote) na tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote).

Zitto: Wanasiasa jivueni minyororo ya mwaka 2020

Aidha amesema Serikali imesamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi TZS 30,000 na kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala.

Mbali na hayo, Waziri Nchemba amekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara imeunda tume ya watu 200 inayotumia mabilioni ya pesa na kubainisha kuwa, wataalam wa Wizara ya Fedha na Mipango wanaohusika na maswala ya Bajeti na Sera wamefanya mapitio wakiwa ofisini kama sehemu ya majukumu yao ya kila siku.

Send this to a friend