Serikali yahamasisha vijana kunywa pombe

0
50

Shirika la kitaifa linalosimamia ushuru nchini Japan (NTA), limeandaa shindano maalum la kitaifa ili kupata mawazo yatakayosaidia vijana wengi kuwa na hamasa ya kunywa pombe zaidi.

Mamlaka ya Japan imesema takribani nusu ya vijana nchini humo hawanywi pombe ukilinganisha na watu wazima, hatua ambayo imeathiri ushuru wa nchi hiyo.

‘Sake Viva’ ni kampeni inayotarajia kuja na mpango wa kufanya unywaji kuvutia zaidi ili kukuza ushuru katika tasnia hiyo.

Ifahamu idadi ya mbwa na paka wanaoliwa kwa mwaka China

Shindano hilo linawataka vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 39 kushiriki mawazo yao ili kueta hamasa miongoni mwa vijana wenzao.

Tovuti ya kampeni hiyo imesema, soko la pombe la Japan linapungua ikilinganishwa na idadi kubwa ya watu walioko nchini humo.

Kulingana na gazeti la The Japan Times, mapato ya ushuru kutoka kwenye pombe yamepungua kutoka asilimia 5 ya mapato yote mnamo 1980, mpaka kufikia asilimia 1.7 mnamo 2020.

Send this to a friend