Serikali yaitaka TCU kuchunguza tuzo zinazotolewa na vyuo vya nje

0
39

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuchunguza ubora wa elimu pamoja na kutuma timu ya wataalamu kuhakiki tuzo zinazotolewa na baadhi ya vyuo nje ya nchi.

Akitoa agizo hilo jijini Dodoma wakati akizindua bodi hiyo, amesema lengo ni kuwapa taarifa sahihi Watanzania wanaotaka kupeleka watoto wao kusoma vyuo hivyo kwa kuwa ni jukumu la TCU kuwezesha na kudhibiti ubora wa elimu usitetereke.

“Lengo si kuzuia wanafunzi kwenda kusoma kwenye vyuo hivyo bali kutoa taarifa kwa Watanzania kuhusu ubora wa tuzo zinazotolewa na vyuo hivyo hasa vinavyofundisha masuala ya udaktari, nimeshaongea na balozi mbalimbali, timu iende na katibu mkuu kuangalia baadhi ya vyuo vikuu duniani ili kuhakiki,” amesema.

Aidha, amesema kuna baadhi ya vyuo vinafundisha elimu ya udaktari kwa njia ya mtandao na kueleza kuwa hana imani kama vinamwandaa vyema daktari kuja kufanya kazi nchini.

Send this to a friend