Serikali yakanusha madai ya Tundu Lissu kuhusu wakurugenzi kuitwa Dodoma

0
39

Ofisi ya Rais-TAMISEMI imesema kuwa wakurugenzi wa halamashauri hawajaitwa Dodoma kukutana na Rais Dkt. Magufuli kupewa maelekezo maalum kuhusu uchaguzi kama ilivyoelezwa na mgombea Urais wa Tanzania (CHADEMA), Tundu Lissu akiwa mjini Musoma.

Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na wananchi wanapaswa kuipuuza kwani inalenga kuwakatisha tamaa wasimamizi wa uchaguzi kwa nia ya kuvuruga uchaguzi na kuharibu amani ya nchi kwa makusudi.

“Wakurugenzi wote wa halmashauri wapo katika vituo vyao vya kazi wakiendelea kutimiza wajibu wao wa kusimamia shughuli za maendeleo na maandalizi ya uchaguzi,” ameeleza Nyamhanga katika taarifa yake.

Send this to a friend