Serikali yakanusha Prof. Kabudi kuhusika na mkataba wa Kampuni ya Indo Power Solution

0
45

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amekanusha shutuma zilizotolewa kuhusu ushiriki wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania katika mchakato wa kumpata mzabuni wa ununuzi wa Korosho ambaye ni Kampuni ya  Indo Power Solution ya nchini Kenya.

Waziri Kakunda amesema kuwa anashanga kuona Profesa Kabudi anatupiwa lawama kuwa ameingiza Serikali mkenge jambo ambalo si kweli kwani wahusika wakuu ni timu ya wataalam kutoa Ofisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kwamba upatikanaji wa zabuni hiyo ulipitia mchakato yote halali kilichotoke ni Serikali kuvunja mkataba baada ya mzabuni kutotimiza masharti yaliyomtaka kulipa ndani ya siku 10 na hata alipoongezewa muda haikutimiza.

Kumuweka mtu ambaye hana makosa yeyote kwenye suala hili na bahati mbaya sana maagazeti karibu yote yakawa yanaandika yakimlaumu kushauri vibaya Serikalijambo ambalo halina ukweli wowote, Kabudi ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria alikuwa mualikwa tu wa kushuhudia hafla ya utiwaji saini mkataba wa Makubaliano baina ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Kampuni ya Indo Power Solution,” alisema Waziri Kakunda.

Kakunda alisema kuwa ni ajabu kwa kumlaumu mtu aliyealikwa na kuongeza kuwa timu ya wataalam iliyohusika inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa anayeshughulikia Viwanda hivyo kumuhusisha Profesa Kabudi ni jambo hili si sawa ni bora hata wangemuhusisha yeye kwa kuwa ndiye Waziri mwenye dhamana na Biashara.

Aidha Waziri Kakunda amesema kuwa ni vyema Watanzania wakaelewa na kutokubali kupotoshwa juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuvunja mkataba na Kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya iliyokuwa imepewa zabuni ya kununua Korosho tani 100 kwa kutofuata masharti ya mkataba.

Alisema kuwa mchakato wa Kuipatia zabuni Kampuni hiyo ulipitia njia mbalimbali zilizohusisha wataalam kutoka pande mbili na kujiridhisha kuwa Kampuni hiyo inavigezo vyote vya vya kupewa zabuni hiyo ya kununua Korosho nchini na kuongeza kuwa pamoja na kuwa imeshindwa kutimiza masharti ya mkataba uliopelekea Serikali kusitisha mkabata bado inabaki kuwa ni Kampuni halali.

Waziri Kakunda ametoa ufafanuzi huu kufuatia kauli iliyotolewa Bungeni jana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu akimtuhumu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashari, Profesa Paramagamba Kabudi kuitia hasara Serikali kwa kumuhusisha na  mkabata wa makubaliano ya ununuzi wa Korosho tani 100 na kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya ambayo baadae Serikali iliamua kusitisha mkataba wake baada ya Kampuni hiyo kutofuata masharti.

Send this to a friend