Serikali yakusanya milioni 881 kutoka kwa Saniniu Laizer

0
39

Baada ya kuiuzia serikali mawe matatu ya madini ya Tanzanite yenye uzito wa 21.3kg kwa yenye thamani ya TZS 12.5 trilioni, serikali imesema imepata kodi TZS 881 milioni kutoka kwenye biashara hiyo.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akieleza mafanikio ya serikali katika miaka mitano kwenye sekta ya madini.

“Serikali kwa kipindi hicho chote kwa mawe haya matatu ya Saniniu imeshaingiza milioni 881 kama kodi,” amesema Dkt. Abbasi.

Amebainisha kuwa kufanikiwa kwa mchimbaji huyo kumetokana pia na ujenzi wa ukuta katika mgodi wa Mererani kwani awali wachimbaji waliweza kutorosha madini na kwenda kuyauza kwenye masoko yasiyo rasmi.

Amesema mafanikio mengine ya sekta hiyo ni pamoja na ujenzi wa masoko ambayo yamewezesha kudhibiti utoroshwaji wa madini, huku akitolea mfano Soko la Madini Geita ambalo limeongeza mapato ya serikali kutoka TZS 878 milioni kabla ya soko, hadi TZS 2.6 bilioni baada ya soko.

Amewataka Watanzania kuwapuuza wale wote wanaobeza juhudu za serikali, kwani ndio hao hao waliokuwa wakisema serikali itashtakiwa kwa kubadili sheria ya madini na kuzuia usafirishaji wa makinikia.

Send this to a friend