Serikali yaondoa ‘expire date’ kwenye vitambulisho vya Taifa

0
66

Serikali imeondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya kanuni za usajili na utambuzi wa watu.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na hali ya utolewaji wa vitambulisho hivyo.

“Serikali inatoa rai kwa watoa huduma wote nchini wanaotumia utambulisho wa taifa kutoa huduma kwa wananchi hususan taasisi za fedha, benki, kampuni za simu kuendelea kutambua na kutumia vitambulisho vya taifa vilivyo na tarehe ya muda wa ukomo uliopita kwa nkuwa vitambulisho hivyo havitakuwa na ukomo wa matumizi,” amesema.

Abiria sasa kuingia Stendi ya Magufuli kwa kadi za kulipia

Aidha, amesema marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kusisitiza kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe.

Send this to a friend