Serikali imeondoa ulazima wa kuvaa barakoa nchini kutokana na kuendelea kupungua kwa hali ya maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19 duniani kote.
Akizungumza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amebainisha kuwa uvaaji wa barokoa utavaliwa pale inapobidi, mfano kwa wale wenye magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa na kwenye mikusanyiko ya ndani pale inapobidi.
Aidha Waziri Ummy amewataka Watanzania kuendelea kuzingatia unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono ili kupunguza magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kuhara, kipindupindu na magonjwa mengine.
“Ninawata maafisa Afya wa Mikoa na Wilaya zote nchini kuimarisha mifumo ya unawaji mikono kwa maji tiririka au kwa kutumia vitakasa mikono katika ngazi ya kaya, taasisi, sehemu za biashara, stendi za mabasi, mashuleni, nyumba za ibada na maeneo yenye mikusanyiko ya watu,” amesema.