Serikali yapendekeza makosa ya ajali barabarani yapelekwe kwenye makosa makubwa zaidi

0
48

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Askari wa Usalama Barabarani kutokuwa na huruma kwa wazembe wote wanaokiuka sheria za barabarani hata kama gari lenye makosa lina usajili wa namba za Serikali.

Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali mwaka 2024/25 bungeni, amependekeza kuondolewa makosa yote ya ajali za barabarani na kupelekwa kwenye makosa makubwa zaidi kutokana na watu kutoheshimu sheria za usalama barabarani

“Kama sheria zetu ni rafiki sana, tuyaondoe makosa yote ya ajali barabarani kwenye inayoitwa traffic case, tupeleke kwenye makosa makubwa zaidi ikiwezekana huu uwe ni uuaji kama uuaji mwingine kwa maana mtu anayekufyatulia risasi kwa kukusudia ana uhakika kuwa atakujeruhi au kukuua na hata anayefanya uzembe na vyombo vya moto ana uhakika wa kukujeruhi au kuua kwa makusudi kabisa,” ameeleza.

Aidha, amesema katika kipindi cha miaka mitano kutokea mwaka 2019 hadi Mei 2024, ajali za barabarani zilikuwa 10,093 ambapo vifo vilikuwa 7,639 na majeruhi 12,663 huku miongoni mwao wakipata ulemavu wa kudumu.

Send this to a friend