Serikali yapiga marufuku ‘mabonanza’ Shinyanga

0
64

Serikali wilayani Shinyanga imepiga marufuku michezo ya kubahatisha maarufu kama (Mabonanza) na kuagiza jeshi la jadi (Sungusungu) kufanya msako ili kukamata mashine ambazo zinatajwa kuchangia uhalifu pamoja na kusababisha umaskini kwenye baadhi ya familia.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko katika mkutano na viongozi wa jeshi la jadi uliofanyika katika kijiji cha Nyida wilayani humo ambao umejumuisha viongozi wote sungusungu.

Walioondolewa kazini kwa vyeti feki kupewa michango yao ya hifadhi ya jamii

Mboneko amesema baadhi ya wananchi hutumia pesa wanazopata kutokana na mauzo ya mazao na kuzipeleka kwenye mchezo huo, huku baadhi ya vijana na watu wazima wakiuza mashamba yao ili kupata fedha za kucheza bahati nasibu hizo.

Ameongeza kuwa mashine hizo pia zimekuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto kwani baadhi yao huiba fedha ili kushiriki bahati nasibu hizo.