Serikali yapiga marufuku makongamano ya mkesha wa mwaka mpya maeneo ya wazi

0
32

Siku moja kabla ya kuumaliza mwaka 2020, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepiga marufuku makongano au mikutano ya mkesha wa mwaka mpya katika maeneo ya wazi siku ya Disemba 31, 2020.

Waziri George Simbachawene amesema licha ya makomgamamo/mikutano hiyo kuleta mshikamano na umoja kumjua Mungu, lakini hayataruhusiwa katika maeneo ya wazi kutokana na changamoto za kiusalama.

Simbachawene ameelekeza kuwa mikusanyiko hiyo ifanyike kwenye nyumba za ibada na mwisho iwe saa sita na nusu usiku.

Aidha, endapo kutakuwa na ulazima wa kufanyika kongamano au mkutano, taasisi husika itatakiwa kuomba kibali kwa mamlaka zinazohusika, na mkusanyiko huo utatakiwa kufanyika kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Waziri ameonya kuwa mtu au taasisi itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua zinazostahili.

Send this to a friend