Serikali yapiga marufuku matumizi ya vyandarua kwenye bustani za mboga

0
51

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kusimamia agizo la wananchi kutotumia vyandarua vyenye dawa na kuviweka kwenye bustani za mboga.

Ameyasema hayo Aprili 25 mwaka huu katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kitaifa ambayo yamefanyikia jijini Dar es Salaam.

“Kuanzia sasa Mamlaka za Serikali za Mitaa zisimamie agizo hili, na sasa ni marufuku kutumia chandarua chenye dawa kilichotengenezwa maalum kwa kuzuia malaria kuwekwa kwenye bustani zetu za mboga mboga,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Orodha ya nchi 10 za Afrika zenye mamilionea wengi zaidi wa dola

Aidha, ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuchukua hatua kwa kuanzisha matumizi ya vyandarua vipya vyenye viambata aina ya BPO ili kukabiliana na usugu wa mbu dhidi ya vyandarua vyenye viambata vya dawa aina ya Pareto vilivyokuwa vikitumika nchini ambao umefikia kiwango cha zaidi ya asilimia 70.

Send this to a friend