Serikali yapiga marufuku uvutaji sigara maeneo ya wazi

0
29

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ijulikanayo kama “The Tobacco Products (Regulation) Act, 2003” ambayo imetoa katazo la uvutaji wa sigara hadharani.

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Tumbe, Amour Khamis Mbarouk aliyetaka kujua ni lini Serikali italeta Sheria ya kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani.

Dkt. Mollel amesema sheria hiyo imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali.

Mbali na hayo, ametoa wito kwa wabunge kuwa mabalozi wa udhibiti wa tumbaku katika jamii ili kusaidia wananchi kuepuka magonjwa yasiyoyakuambukiza.

Send this to a friend