Serikali yaruhusu wenye visima kusambaza maji

0
15

Serikali imeruhusu matumizi ya maji ya visima binafsi na vya umma vitumike ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi bila kikwazo chochote hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Juma Aweso wakati alipotembelea eneo la matengenezo ya bomba kubwa la inch 72 katika kata ya Wazo, jijini Dar es Salaam ambalo ni sehemu ya kimkakati ya kuongeza msukumo wa maji katika jijij hilo ili kukabiliana na hali ya kina cha maji kupungua.

Kijana akamatwa kwa tuhuma za kuiba mtoto tangu mwaka 2020

Amesisitiza kuwa Serikali ipo bega kwa bega na wananchi wa Jiji la Dar es salaam na Pwani katika kipindi hiki, na kuitaka Mamlaka ya Maji (DAWASA) kuhakikisha migao ya maji iliyowekwa inafuatwa bila ubabaishaji ili kutoa haki kwa kila mwananchi kuhifadhi maji ya kutosha wakati huu.

“Ni bayana Wizara inayo mipango ya muda mfupi ikiwemo kuanza kutumia maji ya mradi wa maji Kigamboni ambao utawashwa Oktoba 30. Mradi huu unatarajiwa kuzalisha takriban lita milioni 70 za maji ambazo zitasambazwa Kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji,” amesema Waziri Aweso.

Ameongeza kuwa hivi karibuni utiaji saini wa kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa maji Kidunda utafanyika mwezi Novemba mwaka huu ambao utakuwa suluhisho la kudumu la upatikanaji wa maji ghafi katika Mto Ruvu, kwani litatumika kukusanya maji wakati wa mvua na maji hayo yatatumika nyakati za kiangazi.

Send this to a friend