Serikali yasajili miradi ya trilioni 17, yaweka rekodi ya ajira

0
50

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Januari, 2023 Serikali imesajili jumla ya miradi ya uwekezaji 537 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7,222 (TZS trilioni 17).

Amesema hatua hiyo imetokana na kuboreshwa kwa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kuimarisha kituo cha Huduma za Mahala Pamoja ili kuvutia wawekezaji kwa kupunguza kero na kurahisisha utoaji huduma.

Ameongeza kuwa ongezeko la usajili wa miradi hiyo unatarajia kutoa ajira takribani 92,770 “kiwango hiki ni kikubwa kuwahi kuandikishwa katika kipindi chochote tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961.”

Dar es Salaam ya 85 kati ya majiji tajiri zaidi duniani

Aidha, amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) imefanikiwa kusajili miradi 38 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 139.70 (TZS bilioni 329) na mauzo nje yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 191.04 (TZS bilioni 450).

“Miradi hiyo ni mahsusi katika sekta zinazozalisha bidhaa zitokanazo na Kilimo, bidhaa za viwandani, bidhaa za mifugo, bidhaa za kemikali, bidhaa za madini na bidhaa za misitu” amesema

Send this to a friend