Serikali yasema asilimia 90 ya vijiji vimefikiwa na umeme

0
35

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kufikia mwaka 2024 mkoa wote wa Singida utakuwa na umeme ikiwa ni sehemu ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha umeme unafika nchi nzima kufikia mwaka 2025.

Akuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, Rais Samia amesema Serikali imepeleka umeme kwenye vijiji kwa asilimia 90 na kabla ya mwaka 2025 itavifikia vijiji 4,071 vilivyobakia.

“Tunatarajia mwaka kesho katikati Singida yote kama mkoa itakuwa inawaka umeme. Niwapongeze sana wana-Singida, na hii itakuwa kabla ya kipindi tulichowekewa na ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwamba tupeleke umeme nchini kote ifikapo 2025,” amesema.

Serikali yatoa bilioni 10 kuimarisha miundombinu ya umeme

Aidha, Rais Samia ameagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha inatafuta fedha na kufanya marekebisho katika eneo la Sekenke lililopo mkoani humo ili magari yaweze kupita vizuri bila kusababisha ajali.

Ikiwa ni hitimisho ya ziara yake mkoani humo, Rais Samia ameshukuru Serikali ya mkoa wa Singida, Wilaya, Chama Cha Mapinduzi na wananchi kwa mapokezi mazuri ya ziara hiyo mkoani humo.

Send this to a friend