Serikali yasema hakuna Homa ya Nyani nchini

0
44

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe amewatoa hofu Watanzania juu ya taarifa za uwepo wa Ugonjwa wa Homa ya Nyani katika maeneo mbalimbali duniani ambapo amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa homa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na wataalamu wa afya wilayani Babati mkoani Manyara amesema kumekuwa na maswali mengi yanayoonesha hofu kwa wananchi kuhusu ugonjwa, na kwamba serikali inafuatilia kwa ukaribu taarifa za kila mgeni anayeingia nchini.

Ummy: Hakuna mgonjwa mpya Homa ya Mgunda

Sichalwe amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapoona dalili za ugonjwa wasioufahamu ili serikali ichukue hatua za haraka kudhibiti ueneaji wa ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Homa ya Nyani husababishwa na wanyama aina ya Nyani na Panya ambapo mgonjwa huwa na mwonekano wa malengelenge hasa maeneo ya mikono yanayofanana na ugonjwa wa Tetekuanga.

Send this to a friend