Serikali yashauri wananchi kuongeza ulaji wa nyama na mayai

0
61

Inaelezwa kuwa pamoja na uzalishaji wa mifugo nchini, bado ulaji wa nyama kwa mtu mmoja kwa mwaka ni mdogo kitaifa ambapo takwimu zinaonesha ni kilo 15 tu kati ya 50 zinazopendekezwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO).

Akizungumza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, ameweka wazi kuwa juhudi zinahitajika kuendelea kuhamasisha wananchi kutumia nyama ya kuku ili kufikia kiwango kinachoshauriwa na FAO.

Aidha, Serikali imebainisha kwamba, kiwango cha sasa cha ulaji wa mayai kwa mtu mmoja kwa mwaka ni 106 wakati mapendekezo ya FAO kiasi kinachotakiwa ni 300.

Amesema takwimu za mwaka 2021/2022 zinaonyesha Tanzania ina kuku milioni 92.8 ambapo kuku wa asili ni milioni 42.7 na kuku wa kisasa ni milioni 50.1 huku kaya zinazojishughulisha na kilimo na ufugaji zikiwa zaidi ya kaya milioni 7, kati ya hizo kaya, zaidi ya milioni 4 sawa na asilimia 55.3 wanafuga kuku.

Ulaji wa nyama kwa sasa ni kilo 15 kwa mtu kwa mwaka, aidha kati ya hizo ni kilo mbili tu zinatokana na nyama ya kuku, hali kadhalika ulaji wa mayai kwa sasa.

Send this to a friend