Serikali yatangaza jina jipya la Hospitali ya Mirembe

0
40

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kubadilisha jina la Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe na kuitwa National Instititue for Mental Health.

Amesema hayo leo katika semina maalum iliyoandaliwa kwa Wabunge wa Bunge la Tanzania kupata elimu ya masuala ya afya ya akili, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).

Mazoea haya ya kila siku yanaweza kuharibu figo zako

“Tunakwenda kubadili jina la Hospitali ya Mirembe ili kujenga taswira mpya ndani ya jamii kwenye huduma zinazotolewa pale, mtu anaweza kwenda pale kutibiwa hata Malaria, lakini jamii inamuita ‘chizi’. Tunataka Mirembe iitwe National Instititue for Mental Health,” amesema

Ameongeza kuwa “Tunataka Hospitali ya Mirembe ifanye kampeni za hamasa na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya afya ya akili, matibabu, tafiti mbalimbali za masuala ya afya ya akili pamoja na kufanya mafunzo.

Send this to a friend