Serikali yatangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Marburg nchini

0
4

Wizara ya Afya imetangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Virusi vya Marburg (MVD) nchini .

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya imesema wagonjwa wawili walithibitika kuwa na maambukizi mkoani Kagera, ambapo kwa bahati mbaya wagonjwa hao walifariki wakati wakipatiwa matibabu.

“Kitaalamu na kulingana na kanuni na taratibu za Shirika la Afya Duniani (WHO), tumekidhi vigezo vya kutangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa MVD. Hivyo basi, leo Machi 13, 2025, ninatangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa MVD nchini, imesema taarifa iliyotolewa na Waziri Jenista Mhagama.

Aidha, Taarifa hiyo imeisisitiza jamii yote kuendelea kuwa makini hata baada ya kutangazwa kumalizika kwa mlipuko huo kwa kuzingatia hatua zote za kujikinga , ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, au kutumia vitakasa mikono (sanitizer).

Send this to a friend