Serikali yatangaza mlipuko wa Kipindupindu Ilala, Dar es Salaam

0
71

Wizara ya Afya imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri ya Ilala jijini Dar es Salaam huku watu 10 wakithibitika kuwa na ugonjwa huo.

Taarifa imeeleza kuwa ugonjwa huo uliripotiwa kwa mara ya kwanza Aprili 20, 2023 eneo la Kivule ambapo watoto wawili kutoka familia moja, akiwemo mwanafunzi mmoja kutoka shule ya msingi Kivule walithibitika kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Mbali na watoto hao, watu wanne pia walithibitika kuwa na dalili za ugonjwa huo, ambapo kati yao wanaume ni wawili na wanawake wawili.

“Energy drinks zinavyosababisha matatizo ya moyo” – JKCI

“Dalili za ugonjwa huo zilianza kuonekana kuanzia Aprili 19, 2023. Visa vyote vinne vya ugonjwa huo wa mlipuko vimetokea kwa wanafamilia wanaoishi kaya moja kata ya Kivule mtaa wa 10.

Katika visa hivyo vyote vinne vimetoka kaya moja, kwa sasa wagonjwa hao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kivule,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa visa vitatu vipya vimeripotiwa katika maeneo ya Tabata, Ilala na Buguruni lakini mpaka sasa hakuna vifo vilivyotokea.

Chanzo: Mwananchi