Serikali yatangaza ukomo wa saa za kufundishwa wanafunzi

0
44

Serikali imesema sheria ya elimu haijaweka ukomo wa saa za kufundisha wanafunzi ili kutoa fursa ya mtaala kuwa nyumbufu kulingana na mahitaji maalumu ya ujifunzaji wa wanafunzi wote pamoja na mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ng’wasi Kamani aliyeuliza swali lake kuwa ni kwanini Serikali haijaweka katika sheria ukomo wa saa za kufundishwa.

Akijibu swali hilo Prof. Mkenda amesema mitaala ya elimu ya Msingi na Sekondari imeweka bayana kwa muda (duration) unaopaswa wanafunzi kusoma ambapo mtaala wa elimu ya Msingi, muda wa kusoma elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la pili ni masaa 3 tu kwa siku na kipindi kimoja ni dakika 30.

Uchunguzi wa watoto walionyofolewa macho na ulimi wabaini wauguzi walidanganya

Waziri Mkenda amebainisha kuwa muda wa kusoma kwa darasa la tatu hadi darasa la saba ni saa 6 kwa siku na kila kipindi ni dakika 40.

“Kwa upande wa elimu ya Sekondari muda wa kusoma ni saa 5 na dakika 20 na kipindi kimoja ni dakika 40. Aidha, kwa mwaka wanafunzi hutakiwa kusoma kwa siku 194,” ameeleza.

Send this to a friend