Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mkoani Mara ambazo ni shule ya Sekondari ya Wasichana Mara pamoja na shule ya Amali Butiama (Butiama Technical Sec School).
Fedha hizo zimetolewa ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) mkoani Mara kwa ajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 kuhusu kuongeza uandikishaji wa wananfunzi wa wanafunzi kidato cha kwanza hadi kidato cha nne pia kidato cha tano na sita.
Kati ya fedha hizo jumla ya shilingi Bilioni 4.1 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya sekondari ya Mara wasichana iliyojengwa katika kijiji cha Bulamba kata ya Butimba wilayani Bunda.
Katika shule ya Sekondari ya Mara wasichana serikali imekamilisha miundombinu mbalimbali ikiwemo Jengo lenye vyumba vya madarasa 2, Majengo 3 yenye vyumba vya madarasa 2 na ofisi 1, madarasa 2 na vyoo, maabara ya Fizikia na chumba cha Jiografia, maabara ya Kemia na Biolojia, Jengo la utawala, vyoo vya wanafunzi matundu 16, chumba cha jenereta, bwalo, Nyumba ya mwalimu yenye vyumba 3, nyumba ya mwalimu (2 in 1), mabweni 8, jengo la wagonjwa pamoja na ujenzi wa uzio.








