Serikali yatenga bilioni 9 kukamilisha ujenzi wa vituo vya Zimamoto nchini

0
63

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 9.93 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa vituo saba vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambavyo vimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.3.

Ametoa kauli hiyo Aprili 26, 2023 wakati akifungua vituo vya kisasa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vya Nzuguni na Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya miradi inayozinduliwa katika juma la kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Majaliwa amesema ujenzi wa vituo hivyo ambavyo ni katika mikoa ya Songwe, Simiyu, Kagera, Njombe, Manyara, Katavi na Geita vitasaidia kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za zimamoto na uokoaji kwa kufika eneo la tukio kwa wakati.

Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376

Aidha, Waziri Mkuu amesema miradi mingine inayotekelezwa na Serikali ni ujenzi wa ofisi za kisasa za Jeshi la Zimamoto Temeke jijini Dar es Salaam na vituo vya polisi vya daraja A vya Kigamboni na Wanging’ombe mkoani Njombe.

Majaliwa amelitaka Jeshi hilo lisimamie vizuri matumizi ya fedha za miradi zinazotolewa na Serikali ili kuharakisha mchakato wa utekelezaji wa miradi hiyo muhimu.

Send this to a friend