Serikali yatoa majibu wa wanne waliopimwa Corona Mwanza

0
48

Watu wanne walioshukiwa kuwa na virusi vya Crona mkoani Mwanza wamethibitika kutokuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemele, Dkt Severin Lalika ameyasema hayo alipokuwa katika kituo maalum cha kupokea washukiwa wa magonjwa ya mlipuko kilichopo Buswelu, na amewatoa hofu wananchi kuhusiana na taarifa za kuwepo kwa virusi vya Corona mkoani humo.

Aidha, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt Charles Samson amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya barakoa (masks) ili kujiepusha kupata maambukizi kutokana na uvaaji (wa barakoa) usio sahihi.

Wananchi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu, kwani bado uelewa ni mdogo miongoni mwao.

Send this to a friend