Serikali yaunda tume kushughulikia changamoto za wafanyabiashara

0
36

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameunda tume yenye watu 14 saba kutoka Serikalini na wengine wakiwa ni wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao watashirikiana kwa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara kwa ujumla.

Uamuzi huo umefuatia baada ya Waziri Mkuu kuahidi kuzungumza na wafanyabiashara hao wa Soko la Kariakoo leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kutafuta suluhu juu ya malalamiko yao kwa Mamlaka ya Mapato (TRA), sheria mpya ya usajili wa stoo na urasimu unaofanyika bandarini.

“Timu hii ndani ya wiki mbili inatakiwa ipitie na ichukue yote, waainishe yanayotekelezeka na kwa sababu bunge lipo bungeni na waziri atapata mrejesho wa haya, na wizara yake kupitia taasisi yatachakatwa na mrejesho mtapewa,” amesema.

TRA: Ukamataji unafanyika tunapofanya ukaguzi kujiridhisha

Aidha, ameitaka wizara kufanya mapitio ya sheria na kanuni zote ambazo zimelalamikiwa na wafanyabiashara hao ili kuleta unafuu katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu amesitisha kanuni zote zinazotengeneza mianya ya kero kwa wafanyabiashara mpaka pale zitakapopitiwa upya pamoja na kuwataka wafanyabiashara wote kurejea katika biashara zao ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.

Send this to a friend