Serikali yawaombea ajira vijana wa Tanzania nchini Qatar

0
47

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Saidi Yakubu wamekutana na kufanya kikao pamoja na Balozi wa Qatar hapa nchini, Hussain Ahmad Al Homaid kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Dunia.

Viongozi hao wamefanya kikao cha pamoja leo Juni 23 katika Ofisi za Ubalozi wa Qatar Oyster Bay jijini Dar es Salaam, kufuatia mashindano ya Kombe la Dunia kufanyika nchini Qatar mwaka huu.

Katika mazungumzo yao, wamekubaliana pande zote mbili kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutumia wataalamu wa Tanzania kushiriki maandalizi kabla, wakati na baada ya mashindano hayo ikiwa ni fursa kwa Tanzania kujifunza namna ya kuandaa mashindano ya kimataifa.

Aidha, Yakubu pia ametumia nafasi hiyo kuwasilisha kwa Balozi huyo maombi ya vijana wa Tanzania kupata fursa ya ajira za muda wakati wa mashindano hayo nchini Qatar.

Send this to a friend