Serikali yawaongezea wageni siku 30 kuishi nchini

0
43

Idara ya Uhamiaji Tanzania imeongeza muda wa vibali vya kuishi nchini kwa raia wa kigeni walioshindwa kurejea katika nchi zao kwa siku 30 kufuatia mlipuko wa homa ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya vya Corona ulioikumba dunia.

Akizungumzia uamuzi huo msemaji wa idara hiyo, Ally Mtanda amebainisha kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na baadhi ya mataifa kuweka zuio la muda kwa wasafiri kuingia katika nchini hizo ili kudhibitia maambukizi mapya ya virusi, uamuzi uliopelekea baadhi ya wageni kushindwa kuondoka nchini.

Ameongeza kuwa wageni hao wataendelea kuwepo nchini hadi pale jitihada za kudhibiti virusi vya Corona zinakapoonesha mafanikio makubwa.

Aidha, amewataka wageni wote wanaoingia nchini kutumia mipaka rasmi kwa kuwa maeneo hayo yana vifaa maalumu vya kupima afya za wasafiri hao ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Send this to a friend