Serikali yaziagiza halmashauri zilizokopa benki za kibiashara kurudisha fedha hizo

0
38

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo,amezitaka halmashauri zote nchini kutoa taarifa Ofisini kwake  juu ya uchukuaji wa mikopo kutoka mabenki ya kibiashara.

Agizo hilo Jafo amelitoa leo ofisini kwake jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Jafo amesema kuwa wale wote waliochukua mikopo na hawajaanza kuitumia wairudishe haraka ipasavyo kwani Taasisi zote za Serikali zikiwemo mamlaka za Serikali za Mitaa hazitakiwi kuchukua mikopo kutoka mabenki ya kibiasha.

“Hayo ni maelekezo kutoka katika walaka wa Barua ya Katibu Mkuu Hazina barua ya tarehe 13 /12/2016 barua yenye kumbu kumbu namba CBC.155/233/01 kuwa taasisi zote za serikali na mamlaka za serikali hazipashi kuchukua mkopo kutoka benki za kibiashara” amesisitiza Jafo

Aidha Jafo amesema kuwa halmashauri yoyote itakayo wasilisha taarfa zisizo sahihi itachukuliwa hatua za kisheria.

“Hivyo wito wangu kwa  halmashauri hizo ni kuwasilisha taarfa sahihi kulingana na mikopo waliyo chukua kwani udanganyifu wowote utakao bainika kuwa kuna mikopo ya kimashaka mashaka ambayo haikufuata taratibu sahihi ofisi itachukua hatua mbali mbali za kisheria” amesema Jafo

Hata hivyo Jafo amemtaka Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kusimamia  wakurugenzi wake wote kuhakikisha wanafanya kazi kwa kanuni , sheria na taratibu za kazi zinavyowataka kufanya kazi ili kufikia malengo yanayotakiwa katika utendaji wao.

Jafo amesema kuwa baada ya halmashauri zote kuwasilisha taarfa hizo katika ofisi za TAMISEMI itafanya tathimini na kutoa maelekezo baada ya kupima taarfa zilizo wasilishwa.

Send this to a friend