Serikali yazihimiza benki kupunguza riba ili wananchi wanufaike na mikopo

0
26

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa benki nchini kuendelea kubuni madirisha maalum ya mikopo kwa vijana na wanawake ambao huchukuliwa kuwa ni soko gumu kwa huduma za fedha licha ya kwamba ndio sehemu kubwa ya nguvukazi ya taifa.

Akizunguma katika ufunguzi wa semina ya wanahisa wa benki ya CRDB inayofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ametoa wito wa kushughulikiwa kwa changamoto ya masharti magumu na riba kubwa za mikopo ambazo ni kikwazo kwa walio wengi kuweza kunufaika na mikopo.

TRA: Ukamataji unafanyika tunapofanya ukaguzi kujiridhisha

Aidha, amebainisha kuwa ni asilimia 8.6 tu ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma za benki kwa sasa hivyo ipo sababu ya kuongeza kasi ya kuwafikia wananchi waishio maeneo hayo pamoja na kupunguza riba ili kuwafikia wachimbaji wadogo, wafugaji na wavuvi.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya maboresho ya mazingira ya biashara nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara (Blueprint) ambapo baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na serikali kupunguza urasimu na majukumu kinzani katika taasisi za umma na kupunguza baadhi ya kodi na tozo zisizo na tija.

Send this to a friend