Serikali yazuia ndege za Kenya kutua Tanzania

0
45

Tanzania imezuia ndege za Kenya kutua nchini kwa kufuta kibali kilichokuwa kinazipa ruhusa ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuingia #Tanzania.

Taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA) inaeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baadabL ya Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha ya nchi ambazo raia wake wanaruhusiwa kuingia nchini humo kuanzia Agosti Mosi 2020.

TCAA imesema kuwa imebatilisha kibali kilichokuwa kikiipa ridhaa KQ kutua nchi kutokana na uamuzi wa Kenya hadi hapo itakapoamua vinginevyo.

Kwa barua hiyo ya Julai 31, TCAA imesema imebatilisha mipango yote iliyowekwa kurihusu ndege za Kenya kutua Tanzania.

Kenya inafungua anga lake Agosti Mosi baada ya kulifunga tangu Machi 25 ikiwa ni mkakati wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Send this to a friend