SGR yatoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 20,000

0
51

Rais Dkt. Samia Suluhu amesema Serikali ina lengo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafiri na usafirishaji pamoja na kitovu cha biashara na hilo litafanyika endapo miradi yote inayotekelezwa inasimamiwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Akizungumza leo aliposhiriki katika hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa SGR LOT 6 Tabora – Kigoma Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dkt. Samia amesema mkataba huo wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.21 [TZS trilioni 5.1] utatekelezwa kwa miezi 48 na kufikia mwaka 2026 ujenzi huo utakuwa umekamilika.

“Kwa takwimu zilizopo mradi huu wa SGR [Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa] umeshatoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi zaidi ya elfu ishirini na kulipa mishahara ya dola za Marekani milioni 102 ambazo ni sawa na bilioni 238 za kitanzania. Pia umetoa zabuni za dola za kimarekani milioni 820 kwa Watanzania na kuiwezesha Serikali kukusanya kodi yenye jumla ya dola milioni 450 sawa na TZS bilioni 949 za kitanzania,” amesema.

Rais Ramaphosa anusurika kuondolewa madarakani

Aidha, amesema kukamilika kwa reli hiyo ifikapo mwaka 2027 itasaidia kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji pamoja na kupunguza muda wa safari kama ilivyokuwa hapo awali.

Mbali na hayo Rais Dkt. Samia amefafanua kuwa Serikali haitoacha kukopa pale panapokuwa na faida kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa kuwa mikopo hiyo imesaidia kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.

“Kila pale tunapohisi pana faida tutaendela kukopa. Kwa wanaosema awamu hii imekopa sana waseme pia ndio awamu imejenga sana,”ameeleza.

Send this to a friend