Shabiki aliyejichukulia umaarufu AFCON 2025

0
47

Mabadiliko ya kisasa katika michezo yamewafanya mashabiki kuachana na mbinu za jadi za kushabikia na badala yake kutumia njia mbalimbali za ubunifu kama vyombo vya muziki, michoro, mavazi ya kipekee, ngoma na mbinu nyingine za kuvutia.

Katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea nchini Morocco, mmoja wa mashabiki waliovutia hisia za wengi viwanjani ni raia wa DR Congo, Michel Kuka Mboladinga, anayefahamika kwa jina “sanamu hai”.

Kuka amepata umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wake wa kipekee ambapo husimama bila kusogea wakati wa mechi za timu yake, akiwa ameinua mkono wa kulia juu na macho yakielekezwa angani. Mkao huo unamfanya kufanana na aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa DRC, Patrice Lumumba.

Umaarufu wake umevutia vyombo vya habari, ambapo siku ya Jumanne aliwasili Morocco akiwa ameandamana na msafara wa mamia ya mashabiki wa Congo, huku safari yao ikigharamiwa na Serikali ya nchi hiyo.

Hata hivyo timu hiyo iliondolewa kwenye mashindano baada ya kufungwa bao 1-o na Algeria.

Send this to a friend