Shambulio la waasi lamuua Rais wa Chad

0
39

Rais wa Chad, Idriss Derby amefariki dunia saa chache baada ya kutangazwa mshindi wa Urais kwa muhula wa sita.

Taarifa za kifo cha kiongozi huyo zimetangazwa na jeshi la nchi hiyo ambapo limeeleza kuwa kimetokana na majeraha aliyopata wakati akiongoza jeshi katika mapambano dhidi ya waasi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Rais Déby aliyezaliwa Juni 1952 amekaa madarakani kwa miaka 31 kuanzia mwaka 1990 alipoongoza kung’olewa madarakani kwa Rais Hissène Habré.

Déby alishinda uchaguzi wa mwaka 1996 na 2001 ambapo baada ya hapo aliondoa ukomo wa Urais na akashinda uchaguzi wa mwaka 2006, 2011, 2016 na 2021.

Send this to a friend