Shamte afukuzwa uanachama CCM kwa kukosa heshima

0
71

Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimetangaza kumvua uanachama kada mkongwe wa chama hicho, Baraka Shamte kwa madai ya kutomheshimu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi.

Shamte alionekana juzi kupitia mitandao ya kijamii akihojiwa na vyombo vya habari na kusema haridhishwi na utendaji kazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) hivyo Rais Mwinyi akimaliza miaka yake mitano awapishe wengine wagombee.

Msemaji wa chama, Catherine Peter amesema kutokana na kauli aliyoizungumza chama kimemvua uanachama kwa kuwa ameshindwa kuzingatia matakwa ya katiba ya chama hicho inayomtaka kila mtu kuheshimu watu.

“Alikuwa anaheshimika kulingana na umri wake, lakini amekosa sifa kwa kuzingatia kifungu cha 8(1) cha katiba ya chama chetu kinachosema, mtu yeyote aheshimiwe, Baraka Shamte amekosa sifa kwa kushindwa kuheshimu watu, tena kiongozi namba moja Dkt. Hussein Mwinyi,” amedai.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mussa amethibitsha mzee huyo kuvamiwa na watu wasiojulikana, na kusema jeshi limeanza uchunguzi wa tukio hilo.

Send this to a friend