Sheria 6 za usalama wa mwili unazopaswa kumfundisha mtoto wako

0
60

Usalama wa mtoto wako unapaswa kuwa kipaumbele chako cha kwanza, na ni muhimu sana kumfanya mtoto wako afahamu na kumuelimisha kuhusu sheria za usalama wa mwili.

Kwa mzazi na mtoto, mazungumzo haya yanaweza kuwa ya kufadhaisha au hata kuogopesha, lakini kuyaepuka kunaweza kumdhuru mtoto wako.

Hizi ni sheria 6 za usalama wa mwili unazopaswa kumfundisha mtoto wako

1. Mwili wangu ni mwili wangu na ni mali yangu

Mfundishe mtoto wako kusema “Hapana”. Ikiwa hataki kumbusu au kumkumbatia mtu anapaswa kuwa na uwezo wa kusema hapana kwa mtu huyo.

2. Nina usalama

Mfundishe anaweza kuwaamini watu watano. Tengeneza orodha ya watu 4-5 anaoweza kuwaamini, ambao pia anaweza kuja na kuwaambia ikiwa anahisi wasiwasi, hofu au kutokuwa na uhakika.

3. Jina sahihi la sehemu za siri

Mfundishe jina sahihi la sehemu za siri. Mfundishe hakuna mtu anayeweza kugusa sehemu zake za siri na hakuna mtu anayepaswa kumuomba aziguse. Anaweza kuja na kuwaambia watu anaowaamini kila wakati ikiwa anajisikia vibaya kuhusu hilo.

4. Mguso salama na usio salama

Mfundishe akiwa na umri mdogo karibu miaka miwili na nusu hadi miaka mitatu, ili kutofautisha kati ya mguso salama na usio salama. Mfanye aelewe mguso salama kama vile kukumbatia, kutoa tano, hiyo itwafanya ahisi kupendwa, salama na awe huru. Mguso usio salama humfanya asiwe na raha na asijihisi salama.

5. Ishara za tahadhari

Mfundishe ishara za tahadhari za mapema. Iwapo anahisi kuogopa au kutokuwa salama. Anaweza kutokwa na jasho jingi, tumbo kuuma, kutetemeka na moyo wao unaweza kupiga haraka.

6. Hakuna siri za mwili

Mfundishe hapaswi kamwe kutunza siri zozote zinazomfanya asiwe na amani au ajisikie vibaya kuhusu hilo. Mfundishe anapaswa kuja na kuwaambia watu salama au anaowaamini ikiwa anahisi kutokuwa salama.

Send this to a friend