Sheria kuzuia mtuhumiwa kukamatwa kabla ya upelelezi haujakamilika

0
25

Hivi karibuni Tanzania itashuhudia mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa kesi za jinai baada ya Bunge kupitisha muswada wa mabadiliko ya sheria ambapo pamoja na mambo mengine unataka mtuhumiwa akamatwe pindi upelelezi ukiwa umekamilika.

Mabadiliko mengine katika muswada huo ni yale yanayozuia mtu aliyeachiwa kwa amri ya mahakama baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka kusema hana nia ya kuendelea na kesi, kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa sawa na la mwanzo.

Hata hivyo, sheria imetoa upendeleo kwamba matuhumiwa ataweza kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa sawa na la mwanzo endapo tu upelelezi umekamilika, na sharti usikilizwaji wa kesi uanze mara moja.

Mabadiliko yako ambayo yapo katika Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na.7) wa Mwaka 2021 uliopitishwa na Bunge la Tanzania Februari 7, 2022 yamepongezwa na wabunge kwamba yatakwenda kuharakisha utoaji haki.

Mbali na hilo, mabadiliko hayo pia yatapunguza msongamano wa wamahabusu kwa kuhakikisha kila anayekamatwa upelelezi umekamilika, na kupunguza gharama kubwa ya kuendesha magereza kutokana na idadi kubwa ya mahabusu.

Kwa sheria ya sasa, mtuhumiwa anaweza kuachiliwa na mahakama, akakamtwa tena, akaendelea kusota rumande wakati upelelezi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ukiendelea.

Kufuatia kupitishwa kwa muswada huo, hatua inayosubiriwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutia saini ili uweze kuwa sheria na uanze kutekelezwa.

Send this to a friend