Shirika la Afya Duniani kuifanyia majaribio dawa ya corona ya Madagascar

0
53

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limekubali kuifanyia majaribio ya binadamu dawa inayoripotiwa kutibu corona inayozalishwa nchini humo.

Rais Rajoelina amesema WHO imetoa ushirikiano huo baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu (wa WHO), Dkt. Tedros Adhanom.

Dawa hiyo (COVID Organic-CVO) inatengenezwa kutoka katika mmea unafahamika kwa jina la Artemesia Annua wenye asili ya China ambao uliingizwa nchini humo miaka ya 1970 kwa ajili ya kutibu malaria.

Afya: Ifahamu dawa kutoka Madagascar inayoripotiwa kutibu corona

Tayari dawa hiyo imesambazwa na/au imeanza kutumiwa katika baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo Visiwa vya Comoros, Guinea Bissau, Equatorial Guinea, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Liberia, Niger, Tanzania, Nigeria, Senegal na Chad.

Hadi sasa Madagascar imeripoti visa 405 vya maambukizi ya virusi vya corona, ambapo kati ya hivyo, watu 131 wamepona huku wawili wakifariki dunia.

Send this to a friend