Shirika la Afya Duniani linachunguza ugonjwa ulioua watatu Lindi

0
13

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema majibu kamili ya ugonjwa ulioibuka mkoani Lindi yatapatikana, kwakuwa Tanzania ina uwezo wa kuchunguza magonjwa ambukizi na hatarishi.

Ameyasema hayo leo mara katika ufunguzi wa Maabara ya Afya ya Jamii ya Kibong’oto wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

Waziri Ummy amesema tayari wataalamu wa Tanzania wameungana na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kuchunguza ugonjwa huo na kuwa wizara itaendelea kuboresha huduma za maabara kwa kununua vifaa mbalimbali vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa.

Naye Dkt. Mpango ameitaka Wizara ya Afya kuendelea kuimarisha mfumo wa ufuataliaji wa mwenendo wa magonjwa ya kuambukiza hasa magonjwa hatarishi ili kupunguza athari zinazoweza kutokea kwa wananchi kutokana na magonjwa hayo.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini magonjwa na kupata tiba mapema.

Send this to a friend