Shirika la Fedha la Kimataifa kuwasaidia Wamachinga na Wanawake waliopo sekta binafsi

0
11

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (International Finance Cooperation – IFC), Makhtar Sop Diop amemuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kwamba watashirikiana na Tanzania kwa lengo la kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

Diop ametoa ahadi hiyo leo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma alipofika na kufanya mazungumzo na Rais Samia ambapo pamoja na mambo mengine kutokana na utendaji mzuri wa kazi katika kuwaletea maendeleo watanzania, ikiwa ni pamoja na kukua kwa uchumi na kusimamia mfumuko wa bei nchini Tanzania.

Amemfahamisha Rais Samia kwamba Shirika hilo litaendelea kushirikiana na sekta binafsi nchini Tanzania, pamoja na kuangalia namna ambayo wanaweza kuwasaidia wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) na kuwawezesha kiuchumi wanawake wanaofanya kazi katika sekta binafsi.

Eneo jingine ni kuimarisha sekta ya usafiri nchini hususani usafiri wa majini, kuwajengea uwezo wawekezaji katika miradi mikubwa ya ujenzi wa makazi pamoja na uwekezaji zaidi katika elimu na afya.

Kwa upande wake Rais Samia ameipongeza IFC kwa ushirikiano mkubwa inayoutoa kwa Tanzania katika kuunga mkono jitihada zake za maendeleo na kuihakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Shirika hilo katika kutekeleza majukumu yake hapa nchini.

Send this to a friend