Shirika la ndege Japan kukodisha nguo kwa wasafiri kupunguza mizigo

0
31

Shirika la ndege la Japan Airlines limezindua jaribio la kutoa huduma inayowaruhusu wasafiri kuagiza nguo wanazohitaji kwa ajili ya likizo yao nchini Japan, na lengo la kupunguza mizigo kwenye ndege.

Huduma hii inawawezesha wasafiri kuagiza seti za nguo za kukodisha, zikiwa na mitindo tofauti na zinazolingana na majira ya mwaka, na kuzipokea katika hoteli wanazokaa. Baada ya kumaliza likizo, nguo hizo huchukuliwa, kusafishwa, na kurudishwa katika mfumo wa huduma hiyo.

Huduma hii, inayojulikana kama ‘Any wear Anywhere,’ inalenga kusaidia wasafiri kuepuka kubeba nguo nyingi wanapokwenda nchini humo na inaweza kuwa njia rahisi ya kuhakikisha wanavalia vizuri kulingana na hali ya hewa na shughuli zao wakati wa likizo.

Ndege yageuza safari baada ya abiria kupata ugonjwa wa kuharisha

Japan Airlines inakusudia kutoa huduma hii hadi mwisho wa Agosti 2024 na inatarajia kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa kupunguza uzito wa ndege, hivyo kuokoa matumizi ya mafuta.

Send this to a friend