Shisha na sigara za kielektroniki zinavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume

0
49

Wataalamu wameeleza tahadhari kubwa kuhusu uvutaji wa shisha na sigara za kielektroniki, inayojulikana kama E-sigara, na haswa kwa wanawake wajawazito kutokana na hatari kubwa ya magonjwa inayohusiana na matumizi ya bidhaa hizi.

Uvutaji wa shisha na E-sigara unajulikana kusababisha madhara makubwa kwa mapafu kwa sababu bidhaa hizi zinavyo tumbaku yenye sumu ambayo inaweza kusababisha magonjwa kama saratani ya mapafu, kibofu, na mdomo, pamoja na magonjwa ya moyo ya muda mrefu.

Daktari mtaalamu wa masuala ya ulinzi wa mtoto na afya ya umma, Katanta Simwanza, ameelezea jinsi uvutaji wa shisha na sigara hizo unavyoathiri mfumo wa uzazi kwa wanaume na wanawake.

“Shisha na tumbaku zote zina nikotini na huathiri wanawake, haswa wajawazito. Nikotini inaweza kupunguza ubora wa placenta na kuzuia mtiririko wa damu kwenye placenta, ambayo inaweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto kabla ya wakati au uzito mdogo wa kuzaliwa,” amesema.

Mkuu wa Wilaya ashitakiwa kwa kutusi na kukaweka mahabusu watumishi

Amesisitiza kuwa uvutaji wa sigara unaweza kuchangia kifo cha ghafla cha watoto wachanga siku chache tu baada ya kuzaliwa.

Kwa upande mwingine, ameeleza kuwa uvutaji wa shisha na bidhaa zingine za tumbaku husababisha uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume kwa wanaume na huathiri ubora wa manii, na pia husababisha mbegu hizo kuwa dhaifu katika mchakato wa urutubishwaji.

Send this to a friend