Shujaa Majaliwa aanza mafunzo chuo cha Zimamoto Tanga

0
49

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali John Masunga amesema kuwa tayari jeshi hilo limempokea kijana aliyeokoa abiria wa ajali ya ndege ya Precision Air, Majaliwa Jackson Samweli ikiwa ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema Majaliwa anatarajia kuanza mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji pamoja na ya Uaskari katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga.

“Ikumbukwe kuwa tarehe 06 Novemba, 2022 ilitokea ajali ya kuanguka kwa Ndege ya Precision Air katika Ziwa Victoria, ajali ilisababisha majeruhi na vifo. Majaliwa alionesha ujasiri wa hali ya juu, kwa kuokoa wahanga 24 wa tukio hilo.” ameandika.

Aidha, jeshi hilo limetoa pole kwa wafiwa na wahanga wa ajali hiyo pamoja na kuwasihi wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kuokoa maisha ya watu na mali dhidi ya majanga mbalimbali.

Send this to a friend