Shujaa wa Hotel Rwanda amwomba radhi Kagame, aachiwa huru

0
43

Shujaa wa filamu ya Hollywood inayojulikana kama Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina (68) ameachiliwa kutoka jela mjini Kigali miaka miwili baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 kwa kosa la ugaidi.

Rusesabagina amemuomba msahama Rais Paul Kagame na kukubali kujiepusha na siasa za Rwanda pamoja na kuahidi kuishi maisha yake yote kwa utulivu nchini Marekani.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo amesema hukumu ya Rusesabagina imebadilishwa kwa amri ya Rais.

Nchi 9 za Afrika zilizotembelewa na watalii wengi zaidi mwaka 2022

Tangazo hilo linakuja wiki mbili baada ya Kagame kusema kuwa Kigali inatafuta kusuluhisha kesi ya Rusesabagina, ambayo Qatar na Marekani zimeonesha jitihada katika kutatua kesi hiyo pamoja na mashirika ya kutetea haki za ulimwengu.

“Paul Rusesabagina na (mshtakiwa mwenza) Callixte Nsabimana wamebadilishiwa vifungo vyao kwa amri ya Rais, baada ya kuzingatia maombi yao ya kuhurumiwa,” amesema Makolo.

Hukumu za watu wengine 18 waliopatikana na hatia ya makosa ya ugaidi pamoja na Rusesabagina mnamo Septemba 2021 pia zimebadilishwa.

Send this to a friend