Shule kuwatoza faini ya TZS 5,000 kwa siku wazazi wa wanafunzi watoro

0
70

Shule ya Sekondari Muhalala, wilayani Manyoni mkoani Singida, imeweka utaratibu mpya wa kuwatoza faini ya Shilingi 5,000 kwa siku wazazi au walezi wa wanafunzi watoro, ikiwa ni hatua ya kudhibiti tatizo la utoro shuleni.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano maalum ulioshirikisha uongozi wa shule, walimu na wazazi, uliolenga kujadili sababu za kupungua kwa idadi ya wanafunzi watakaohitimu kidato cha nne mwaka huu, tatizo ambalo limeelezwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na utoro wa wanafunzi.

“Tumechoka kuona ndoto za watoto zikipotea kwa sababu ya utoro. Sheria hii imelenga kukuza nidhamu na kuinua ufaulu,” amesema Mkuu wa Shule, Mwalimu Mashaka Ringi.

Amesisitiza kuwa utekelezaji wa hatua hiyo utaanza mara moja kwa wazazi au walezi watakaokiuka.

Send this to a friend